Wednesday, May 31, 2023

Bwana Nimerudi Tena Lyrics by Tag Forest

 BWANA NIMERUDI TENÀ


Bwana, nimerudi tena

Yesu Nakushukuru

Wengine Sijui, ila mimi Bwana

Nimejua umenitendea.(X2)


Bwana, nimerudi tena

Yesu Nakushukuru

Mengine sijui, ila Hili Bwana

Nimejua umenitendea


Nimeomba mengi umenijibu moja

Umetutendea wengi mimi nimerudi

Japo mengine bado, ila natambua

Dhamani ya Hili moja ulilolitenda.


Wale wengine kenda mimi Sijui

Ila nachojua, kwangu umetenda

Mengine sijui ila hili Bwana 

Nimejua umenite-ndea


Mimi ni msamaria tu 

Mtu wa makabila mengine 

Wala sikustahili haya uliyonitendea 

Wengine sijui wanaona nini 

Ila mimi Bwana, ninauona wema wa ajabu.


Wenye ukoma, Tulikuwapo 

Na neno lako, halikufanya makosa 

Wengine sijui, ila mimi Bwana 

Nimejua umenitendea.


Wenye dhambi,Tulikua wengi 

Na damu yako, ikanitakasa 

Wengine sijui, ila mimi Bwana

Nimejua umenitendea.


Utukufu 

Kwako Tu 

Na Heshima 

Zako Tu 

Umenitenda Wema 

Umenitenda vyema 

Umenitendea weee-maa tu.

https://youtu.be/NSGmmnzVCLk


No comments:

Post a Comment